Tanzania Commission for AIDS @tacaidsinfo
179 Posts
2k Followers
1k Following
Ukurasa rasmi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania - (TACAIDS) kupata machapisho bure 👉👉 http://library.tacaids.go.tz/
179 Posts
2k Followers
1k Following
Ukurasa rasmi wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania - (TACAIDS) kupata machapisho bure 👉👉 http://library.tacaids.go.tz/
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Dkt. Anna Mghwira anawakumbusha vijana wa Kitanzania kuwa UKIMWI bado upo hivyo ni muhimu wachukue tahadhari ya kujikinga na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI vile vile kutumia fursa ya jukwaa la Tamadha la WASAFI 2019, Kupata Elimu ya Kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI pamoja na kupima ili kujua afya zao.
57 7
KUPIMA VVU NI JAMBO JEMA KABISA Kuna faida nyingi sana za kupima Virusi Vya UKIMWI, Moja kubwa zaidi ni kujua hali yako ya maambukizi ya VVU ili uweze kuwa kwenye nafasi nzuri ya kupanga mipango mbali mbali ya maisha. *KUMBUKA:* Kama utagundulika kuwa unaishi na maambukizi ya VVU basi utakua kwenye nafasi nzuri ya kupata huduma za matibabu ambazo zitakuwezesha kuishi kawaida kabisaaa ukiwa mwenye afya njema NA kama utagundulika kuwa hauna maambukizi ya VVU basi utakua kwenye nafasi nzuri ya kujikinga na maambukizi ya VVU na kukufanya uweze kupanga mipango yako ya maendeleo Kupima VVU ni ufunguo wa kukufanya uwe na nafasi nzuri ya kufanya maamuzi katika maisha yako Asante kwa @wasafiifestival2019 @wasafi._tv @wasafifm kwa support ya kutoa elimu ya VVU na UKIMWI kwa vijana kupitia msimu huu wa #wasafiFestival2019 #WasafiFestival2019UKIMWIBadoUpo
63 5
Serikali inanedelea kutenga bajeti kwa ajili ya kusaidia shughuli mbali mbali zinazolenga kupunguza maambukizi ya VVU. Naibu Waziri. Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeratibu watu wenye ulemavu. Mhe. Stella Ikupa anaeleza kwa kina, msikilize hapo juu. Asante @wasafiifestival2019 kwa support
48 2
Watumishi wa kada ya afya wakisikiliza mada mbali mbali wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo juu ya utekelezaji wa sheria ya UKIMWI ya mwaka 2008 kilichofanyika Mkaoni Dodoma katika Ukumbi wa chou cha Mipango tarehe 24 Julai 2019.
83 8
Mratibu wa UKIMWI wa sekta ya afya, Mkoa wa Tanga Dkt. Selemani Msangi akitoa ufafanuzi kwa watumishi wa sekta ya afya juu yautekelezaji wa miongozo ya utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI Tanzania bara, wakati wa kikao kazi cha kuwajengea uwezo juu ya sheria ya UKIMWI ya mwaka 2008, tarehe 24 Julai 2019.
29 2
Meneja wa Uraghibishi na mawasiliano kutoka baraza la taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) Bw. Gregory Kamugisha, akiwasilisha mada ya haki na wajibu kwa watu wanaoishi na VVU (WAVIU) Tanzania, katika kikao kazi cha kuwajengea uwezo watumishi wa kada ya afya kuhusu sheria ya UKIMWI ya mwaka 2008 na haki za binaadamu, tarehe 24 Julai 2019
25 3
Wadau wanaotekeleza afua za VVU na UKIMWI Tanzania bara, wakisikiliza mawasilisho ya taarifa ya maeneo ya uwekezaji katika utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI Tanzania “Tanzania HIV Investment Case’’ kutoka kwa muwezeshaji, aliyeshiriki kuandaa zana hiyo, tarehe 24 Julai 2019.
41 1
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia UKIMWI (UNAIDS) hapa nchini Dkt. Leo Zekeng, akizungumza na wadau walioshiriki katika kikao cha uwasilishwaji wa taarifa ya maeneo ya uwekezaji katika utekelezaji wa afua za VVU na UKIMWI Tanzania kwa lengo la kuimarisha Mwitikio wa kitaifa wa Kudhibiti VVU na UKIMWI, tarehe 24 Julai 2019
30 1