Clouds TV 馃嚬馃嚳 @cloudstv
10k Posts
1m Followers
2 Following
Official instagram page for Clouds TV|
10k Posts
1m Followers
2 Following
Official instagram page for Clouds TV|
#Picha: Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Bi Rukia Muwango (@rukiamuwango_) akiwa kwenye matukio mbalimbali katika wiki ya ukaguzi wa miradi ya #TASAF na mikutano ya hadhara vijiji vya Nachingwea. #CloudsDigitalUpdates | #Nachingwea.
718 2
"Katika jambo kubwa na adhimu kama la Muungano siku zote kutakuwa na mambo ya kushughulikia, asiye mtu kwasababu kuna changamoto ya biashara au jambo lingine lolote akakwambia basi muungano huu haufai, huyo atakuwa na sababu nyingine kwani ili kitu ukiue lazima ukipe jina baya kwanza" January Makamba - Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani dodoma katika warsha kuelekea maadhimisho ya miaka 54 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
481 6
Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde (@anthonymavunde) amekabidhi pikipiki ya magurudumu matatu (BAJAJ) kwa #Mal#Mal#MalkiaWaNguvu Nisse Helga Donald ikiwa ni utekelezaji wa ahadi iliyotolewa kwa mjane huyo wakati wa semina ya #MalkiaWaNguvu mkoani Dodoma. Naibu Waziri Mavunde aliyekuwa mgeni rasmi katika semina hiyo akishirikiana kwa ukaribu na Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi pamoja na Mbunge wa Viti Maalum #MalkiaWaNguvu Halima Bulembo (@halima_bulembo) waliahidi kutoa Bajaj mpya ikiwa imefanyiwa malipo ya vibali vyote kwa Bi Nise ambaye #KovuLaThamani halikumkatisha tamaa bali lilimpa nguvu ya kupenya na kuwa dereva wa bajaj kazi ambayo imezoeleka kufanywa na wanaume, kazi inayomuwezesha kuihudumia familia yake #CloudsMediaGroup inatoa shukrani zake za dhati kwa kila aliyefanikisha hili
1k 6
Kama utacheza kwa kutumia shilingi 25,000 unaweza kupata hiyo milioni 5 ndani ya dakika 60. Hata kama hutashinda hiyo, kitendo cha kucheza kwa kiasi chochote kinachoanzia shilingi 500 kinakupa uwezekano wa kupata milioni 140 kesho. Cheza sasa hivi (kwa #AirtelMoney #TigoPesa au #Mpesa unaenda LIPIA BILI unaweka namba ya kampuni 555111, weka dau, sehemu namba za kumbukumbu unaweka namba zako 3 za bahati), na usisahau neno WEB baada ya namba zako za bahati.
1k 7
Mazingira yakibadilika na wewe unabadilika kukabiliana nayo. Picha imepigwa maeneo ya KINONDONI na @imaninsamila. #Mazingira
2k 19
Naibu Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira na Muungano, Kangi Lugola amefungua warsha ya Muungano kwa wanafunzi wa shule za msingi zilizopo Dodoma iliyolenga kukumbusha misingi ya amani, umoja na uzalendo kwa wanafunzi wa shule za msingi katika kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano zitakazoadhimishwa kitaifa mkoani Dodoma tarehe 26 April. Jumamosi April 21 Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano itaendesha warsha nyingine kwa wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Dodoma ambapo Waziri January Makamba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
404 2
Wanafunzi wa shule ya msingi #Aghakan mapema ya leo wamekata kiu yao ya muda mrefu, kwa kutembelea #CloudsMedia na kujifunza, kujionea na kupata nafasi ya kushiriki katika kipindi cha Tv (Clouds360), pia kuzungumza na wadau na personalities mbalimbali wa hapa #Mjengoni. #AmkaInakubiriDunia
1k 13
鈥淭akwimu zinaonyesha kuwa kila baada ya dakika 12 mtoto mmoja hufariki nchini Tanzania kutokana na utapiamlo ambapo mikoa inayoongoza kwa utapiamlo uliokithiri ni Singida, Arusha na Manyara. Tanzania ni nchi ya 3 Afrika inayoongoza kwa udumavu huku ikishika nafasi ya 10 kidunia kwa udumavu uliokithiri鈥. Peter Serukamba -Mbunge , Kigoma Kaskazini akiwasilisha maoni ya kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii kuhusu makadirio ya bajeti ya wizara ya afya Bonyeza Link kwenye Bio yetu hapo juu kutazama taarifa yote pia subscribe channel yetu ya #YouTube #CloudsMedia.
482 4